Khatibu, Sheikh Khalfan Katundu, katika Khutba yake ametanabahisha kuwa matukio kama vile tukio la "Muslim bin Aqil (RA)" yana umuhimu mkubwa kwa jamii zote za Kiislamu. Kwa mfano, vijana wa Kiislamu nchini Tanzania wanaweza kuelimishwa kuhusu thamani ya ushujaa, utoaji sadaka na kujitolea kijamii na kidini, na kuwa na Mapenzi makubwa kwa Haki na Uadilifu kupitia Hadithi na Hikaya za Matukio mbalimbali ya Karbala.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jamiat Al-Mustafa - Dar-es-salaam - Tanzania, Leo hii (27-07-2025) ilifanya Majlisi ya tukio la kihistoria, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hussein (as) na Mashahidi wote wa Karbala, waliouliwa na kufanyikiwa kila aina ya ukatili katika Ardhi ya Karbala mwaka 61 Hijria na ndani ya Mwezi huu Mtukufu wa Muharram.
Khatibu katika Majlisi hii: Sheikh Khalfan Qasim Katundu, alizungumza kuhusiana na:
"Umuhimu wa Muslim bin Aqil (RA) na tukio la kihistoria la Karbala".
Sehemu ya nukta maridhawa zilizokuja katika khutba hiyo (iliyojikita katika kuelezea historia halisi ya Muslim bin Aqil (RA), na zenye kuacha athari chanya kwa mioyo ya hadhira, ni pamoja na Khatibu kugusia:
1_Ujasiri na imani ya Muslim bin Aqil (RA).
2_Na jinsi tukio la Karbala linavyothibitisha thamani ya kujitolea na kupigania Haki, hata kama utakumbana na mateso makubwa katika njia ya kuipigania Haki hiyo na Ukweli.
Athari ya Tukio Kama Hili
Khatibu alitanabahisha kuwa Matukio kama tukio la Muslim bin Aqil yana umuhimu mkubwa kwa jamii zote za Kiislamu.
Kwa mfano, vijana wa Kiislamu nchini Tanzania wanaweza kuelimishwa kuhusu thamani ya ushujaa, utoaji sadaka na kujitolea kijamii na kidini, na kuwa na Mapenzi makubwa kwa Haki na Uadilifu kupitia Hadithi na Hikaya za Matukio mbalimbali ya Karbala.
Hili ni somo muhimu ambalo linawahamasisha watu kuwa na imani imara na kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki na ukweli na kuwa pamoja na haki popote pale ilipo.
Vilevile, kwa vile maeneo kama Dar es Salaam, Tanzania, ni maeneo yenye mchanganyiko wa tamaduni nyingi, kufanyika kwa tukio hili la Kiutamaduni wa Kidini kunaweza kuwa na athari chanya katika kuimarisha mshikamano wa kidini na kuhamasisha jamii kuendelea kudumisha imani ya Kiislamu kwa njia ya amani.
Hapana shaka kuwa programu kama hizi za Utamaduni wa Kidini, watu kukaa na Kuzungumzia masaibu ya Karbala na kukumbushana yaliyojiri katika Historia ya Kiislamu, zinasaidia katika kuleta umoja zaidi kati ya Waislamu wa Ulimwengu mzima, hususan Waislamu wa Afrika Mashariki, ukizingatia kuwa Waislamu wengi Duniani ni Wapenzi wa Haki na Uadilifu, ni Wapenzi wa Historia ya Kweli, na ni Wapenzi wa Historia sahihi ya Mtume Muhammad (saww) na Ahlul-Bayt wake (as), na Uislamu na Waislamu kwa ujumla walioipigania Dini Tukufu ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) kwa Mali zao na Damu zao kama vile Damu ya Muslim bin Aqil iliyomwagwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu (SWT).
Your Comment